Korea Kaskazini imeripoti kwa Shirika la Afya Ulimwenguni kuwa hakuna kesi ya corona nchini humo.

Hayo yametangazwa na Maafisa wa Korea Kaskazini, katika ripoti ya hivi karibuni iliyowasilishwa kwa WHO kwamba hakuna mtu yoyote mwenye virusi vya corona nchini humo.

Mwakilishi wa WHO wa Korea Kaskazini, Edwin Salvador ameeleza kuwa jumla ya watu 23,121 pekee ndiyo wamepimwa kote nchini humo tangu kuanza kwa janga hilo.

Watu 732 kati yao walipimwa katika kipindi cha kuanzia Machi 26 – Aprili 1, na hakuna aliyekutwa na virusi vya corona.

Korea Kaskazini ilitangaza jana kuwa haitashiriki Olimpiki ya Tokyo ili kulinda wanariadha dhidi ya janga la corona.

Semunyu: Tshibangu amedanganya, aseme ukweli
Young Africans yakataa kubebwa kimataifa