Korea Kaskazini imesema kuwa itaiachia meli ya uvuvi ya Korea Kusini iliYoikamata siku sita zilizopita kwa kuingia katika himaya yake kinyume cha sheria.

Meli hiyo na wafanyikazi wake itaachiliwa katika mpaka wa kijeshi katika bahari, kulingana na taarifa iliyotolewa na shirika la utangazaji la Korea Kaskazini KCNA.

Uamuzi huo wa kuiachia meli hiyo umechukuliwa mara baada ya wafanyakazi  kuomba msamaha kwa kuingia ndani ya bahari ya nchi hiyo na kufanya shughuli za uvuvi bila kibali.

Aidha, hatua hiyo imejiri wakati ambapo kuna wasiwasi mkubwa katika eneo hilo huku pande zote mbili zikifanya mazoezi ya kijeshi ili kuweza kujihami na chochote ambacho kinaweza kujitokea.

Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na Korea Kaskazini, umethibitisha kuwa wavuvi hao waliingia ndani ya maji ya taifa lake kimakosa mara baada ya kukiri kuwa hawakujua kama wamevuka mpaka.

JPM ampa shavu Dkt. Kashillilah
Koeman aeleza sababu ya kutimuliwa Everton, amtaja Giroud