Korea Kusini imesema kuwa Korea Kaskazini imeahidi kufunga eneo lake la kufanyia majaribio ya nyuklia mwezi ujao na itaalika wataalamu wa kimataifa na waandishi wa habari kushuhudia kufungwa kwa eneo hilo.

Hayo yamebainishwa na Ofisi ya rais wa Korea Kusini, ambapo imesema kuwa pia Korea Kaskazini imekubali kubadilisha saa zake kuwa sawa na za Korea Kusini, ikiwa ni ishara nzuri kwa kuwa kwa sasa saa ya Korea Kaskazini iko nusu saa nyuma ya ile ya Korea Kusini.

Aidha, Korea Kusini imeongeza kuwa hatua hizo zinakuja baada ya mkutano wa kihistoria uliofanyika siku ya Ijumaa kati ya viongozi wa nchi hizo mbili.

Hata hivyo, siku ya Ijumaa, kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un na rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in walikutana kufanya mazungumzo ya kuondoa tofauti zao ambazo zimekuwa za muda mrefu.

 

Wanajeshi wanne wauawa nchini Somalia
Mnataka wasipate wateja? waacheni wavae nguo zenye mpasuo ndio- Msukuma