Kiongozi wa juu wa Korea Kaskazini, Choe Son-hui amemtukana kwa kumuita ‘Mjinga’ Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence na kuonya kuwa kutakuwa na maonyeshano ya ubabe wa nyuklia ikiwa mazungumzo yatafeli.
Choe Son-hui amesema kuwa Pyongyang haitaweza kuibembeleza Marekani kwa vyovyote vile ili kuweza kufanikisha mazungumzo.
Siku za hivi karibuni pande zote mbili zimeonya kuwa mkutano wa Juni 12 mwaka huu unatarajiwa kufanyika nchini Singapore unaweza kuahirishwa au kufutwa.
Aidha, Korea Kaskazini imesema kuwa itafikiria tena iwapo itahudhuria mkutano huo ikiwa Marekani itaendelea kusisitiza kuwa iachane na mpango wa silaha za nyuklia.
“Kama mtu ambaye nimehusika kwenye masuala ya Marekani, siwezi kuficha mshangao wangu kufuatia matamshi kama hayo ya kijinga yanayotoka kinywani mwa Makamu wa Rais wa Marekani,”amesema Choe Son-hui
-
Trump amgeuka mshauri wake kuhusu kuifanya Korea Kaskazini kama Libya
-
Marekani yaikomalia Iran kuhusu vikwazo
-
Kim Jong-un azidi kumvuruga Trump
Hata hivyo, Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa Korea Kaskazini inatakiwa kutimiza masharti ya kufanyika kwa mazungumzo hayo.