Korea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kufanya jaribio la kombora lake la masafa marefu ICBM, huku ikitoa onyo kali kwa Marekani kuwa inauwezo wa kushambulia eneo lolote lililopo nchini humo.
Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un amesema kuwa jaribio hilo limebaini kuwa Marekani yote ipo katika rada ya Korea Kakazini na sasa inaweza kushambuliwa wakati wowote kwa makombora hayo.
Aidha, Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa jaribio hilo ni la kijinga na ni kitendo cha kichokozi na cha hatari kilichotekelezwa na utawala wa Korea Kaskazini, ambapo ameongeza kuwa hali kama hiyo isipodhibitiwa inaweza kusababisha athari kubwa kwa jamii.
Hata hivyo, China imeshutumu jaribio hilo huku ikitaka pande zote zinazoshutumiana kuvumiliana na kutoendelea na majaribio hayo kwani yanaweza kusababisha madhara makubwa na kuhatarisha usalama wa eneo husika.