Waziri Mkuu wa Korea kusini, Lee Nak-yeon amesema kuwa kabla ya kukubali mwaliko wa Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un ni lazima kuwepo na masharti yatakayochagiza mazungumzo hayo.
Katika hatua kubwa ya kidiplomasia kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, alimwalika mwenzake wa Korea Kusini kwa ajili ya mazungumzo lakini Rais Moon Jae-in bado hajatoa jibu lolote la kuitikia wito huo.
Aidha, ujumbe huo wa mwaliko umetolewa na dada yake kiongozi wa Korea kaskazini, Kim Jong-un ambaye aliandamana na maafisa wa ngazi za juu zaidi wa Korea Kaskazini kuwahi kutembelea Korea Kusini tangu kumalizika kwa vita vya Korea miaka 60 iliyopita.
Hata hivyo, hatua hiyo haijafurahiwa na Marekani ambayo bado inataka kwanza Korea kaskazini ishinikizwe kuachana na miradi yake ya nyuklia.