Serikali ya India, imekubali kuondoa ushuru wa asilimia 35 kwa Korosho iliyobanguliwa kutoka Tanzania, iliyokuwa ikitozwa awali kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanya ziara ya Kikazi Nchini humo.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akizungumza na Waandishi wa habari akiwa nchini India amesema Korosho itakayoondolewa ushuru, huo ni ile itakayokuwa ikibanguliwa na Kampuni kutoka India iliyopo nchini Tanzania.

”India ina sheria inayotoza kodi ya asilimia 35 kwa korosho yoyots inayongia kwao ikiwa imebanguliwa. Sasa kuna kiwanda tumefungua cha kubangua korosho na tumekubaliana ile itakayotoka kwenye kiwanda hicho haitakuwa inatozwa kodi kama ilivyokua hapo awali,” amesema Waziri Bashe.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemaliza ziara yake ya siku 4 Nchini India na kurejea nyumbani Nchini Tanzania.

Vijana, nashindwa kuwajengea hoja hakuna matokeo - Luhemeja
Serikali kusitisha uuzaji Korosho ghafi nje ya Nchi