Polisi nchini Indonesia imewakamata wafanyakazi wa Kampuni ya dawa ya Serikali Kimia Farma kwa madai ya kuosha vifaa vya kupimia puani ugonjwa wa Covid 19 vilivyotumika na kuvitumia tena.

Inakadiriwa kuwa takriban abiria 9,000 katika uwanja wa ndege wa Kualanamu nchini Indonesia, huenda wamepimwa Corona na vijiti vya pamba vilivyotumiwa na abiria wengine.

Kampuni hiyo sasa inakabiliwa na kesi itakayofunguliwa kwa niaba ya wasafiri.

Mwenendo wa kupima abiria puani umekuwa kama kawaida katika nchi nyingi zilizoathiriwa na janga la corona.

Polisi wanaamini ulaghai huo ulianza tangu, Desemba 2020 katika uwanja wa ndege wa Kualanamu huko Medan, Sumatra Kaskazini.

Mamlaka ya uwanja wa ndege imekuwa ikitumia vifaa vya vipimo vya Covid-19 vilivyosambazwa na kampuni ya serikali ya Kimia Farma.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Mei 6, 2021
Niyonzima: Dakika 90 zitaamua