Kamati ya nidhamu ya Klabu ya Simba SC inayoongozwa na Kamishna wa Polisi wa zamani wa Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova imesukumiwa kesi ya Wachezaji watano wa klabu hiyo ambao wanadaiwa kucheza chinio ya kiwango dhidi ya Young Africans.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Iman Kajula, amesema Simba haifanyi jambo kwa kukurupuka na kila sehemu ina kamati mbalimbali ikiwamo Uchunguzi na nidhamu.

Amesema katika fununu zilizotolewa kuhusu wachezaji hao, linafanyiwa kazi na kupelekwa kwenye kamati ya nidhamu ambayo inawajibu kufanyia kazi na kutoa hukumu pale ambapo kuna bainika kuna makosa.

“Zile fununu au tetesi za nyota hao tayari zinafanyiwa kazi na kamati itakuja kutolea majibu endapo itabainika kuna makosa, viongozi watatekeleza kwa kuchukuwa hatua,” amesema Kajula

“Klabu ya Simba tunaamini kupiga hatua kubwa katika maendeleo ya michezo lazima kuwapo nidhamu sifa ya kwanza kwa mchezaji uongozi hawatafumbia macho mchezaji au mwajiriwa ndani ya klabu hii anayeonesha utovu wa nidhamu.”

Amesema lazima mchezaji au mwajiriwa ndani ya klabu hiyo atahukumiwa kulingana na jambo ambalo amelifanya pindi uchunguzi wa kina na kamati ya nidhamu zitakapojiridhisha.

Kuhusu mrithi wa Robertinho Oliveira ‘Robertinho’, Kajula amesema mchakato unaendelea na siku chache zijazo watamtangaza kocha mkuu pamoja na wa viungo.

Amesema wamepokea CV nyingi za makocha mbalimbali lakini wameweka vigezo vyao na tayari amepatikana, hivyo kinachosubiriwa ni muda wa kumtambulisha rasmi.

“Ni kweli tunahitaji kupata kocha mkuu kabla ya haya mapumziko ya Kalenda ya FIFA kufikia tamati, tungependa juma lijalo tunapokwenda kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Asec Mimosas tuwe tayari tumeshamtangaza kocha wetu,” amesema Kajula.

Mtendaji huyo amewataka mashabiki wa Simba SC kutulia na kuendelea kuunga mkono viongozi na wachezaji kuelekea maandalizi ya mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Asec Mimosas ya lvory Coast.

“Makocha walikuwapo wanaendelea na majukumu yao ya kukisuka kikosi kwa wachezaji wetu kujiandaa na mchezo huo kusaka ushundi na kutafuta alama tatu muhimu za nyumbani,” amesema Mtendaji huyo.

Deco: Xavi Hernandez atabaki kuwa bora
Kwa hili tumepakwa mafuta kwa Mgongo wa Chupa - Bwege