Kiungo wa klabu ya Atletico Madrid, Matias Kranevitter amekiri uwezpo wa tetesi za kuwaniwa na klabu za Chelsea na Arsenal zote za nchini England.

Lakini matajiri wa jiji la London, Chelsea wameongeza kasi ya kumuwania kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa ajili ya kutua darajani mwezi huu wa Januari.

Awali Kranevitter amekuwa akihusishwa na tetesi za kutaka kujiunga kwa Washika Mitutu wa jiji la London na tayari babu Arsene Wenger ameweka mezani ofa kwa ajili yake.

Meneja wa muda wa klabu ya Chelsea, Guus Hiddink inasemekana ameingilia kati dili hilo na anapambana kuhakikisha kiungo huyo anatua katika kikosi cha Stanford Bridge.

Akinukuliwa, kiungo huyo kutoka nchini Argentina, amesema ndoto zake za kutua Emirates zinaweza kuyeyuka kwa sababu Hiddink ameongeza kasi ya mazungumzo.

“Nimekuwa nikisikia malengo ya Hiddink kwangu na kadri ninavyotambua mpango uko hivyo.”

“Ni kati ya makocha wazuri duniani wanaovutua kufanya kazi nao, kila mchezaji anaota ndoto ya kufundishwa na mwalimu wa mfano wake.”

“Kwa nyakati tofauti nimekuwa nikifundishwa na makocha wengine.

Kama kuna siku inatokea Napata nafasi ya kufanya kazi chini yake nitakuwa na furaha kubwa.”

“Lakini kwa sasa bado nipo Atletico. Najisikia furaha kuwa hapa, hakuna tatizo kuwa hapa.”

“Kucheza katika timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa ni kati ya malengo yangu pia. Kila mchezaji anaota mafanikio kama hayo.”

“Ninataraji kuwa katika kiwango hicho cha mafanikio, ninaamini kuna siku nitafikia hatua hiyo, ni suala la kusubiri kuona,” alisisitiza Matias Kranevitter.

Afisa wa Takukuru auawa kikatili
Membe amkosoa Magufuli kuhusu Kubana Matumizi, Safari za nje