Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji imetoa angalizo kwa viongozi wa shirikisho la soka nchini TFF juu ya kumtumia mshambuliaji Mbwana Samatta katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Nigeria.

Uongozi wa Genk umedai Samatta ambaye ameibuka kuwa tegemeo amecheza mfululizo bila mapumziko na hivyo kuhitaji uangalifu zaidi atakapoitumikia Taifa Stars.

“Ukirudi nyuma tangu msimu uliopita utaona Samatta ametumika sana bila kupumzishwa. Tunaomba madaktari na kocha mkuu wamtazame kwa makini wakati wa maandalizi na mechi yenye.” Kiongozi mmoja wa Genk amemuelezea afisa wa TFF anayehusika na timu ya Taifa Stars.

Daktari wa Taifa Stars, Richard Yomba amesema kuwa ni kweli amepokea maagizo ya kumtazama Samatta kwa umakini.

Tayari Samatta ameelekea nchini nchini Nigeria akitokea Ubelgiji huku wachezaji wengine wa Taifa Stars wakitarajia kuondoka kesho alfajiri wakitokea jijini Dar es salaam.

Baada ya kupona mwanzoni mwa mwaka jana, Samatta alicheza ligi ya DR Congo, michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, michuano ya Klabu Bingwa Dunia pamoja na michezo ya kufuzu Kombe la Dunia na Mataifa ya Afrika akiwa na Taifa Stars.

Mwanzoni mwa mwaka huu alijiunga na Genk na moja kwa moja akaingia katika mikimiki ya Ligi bila kupumzika mpaka sasa.

Kevin Yondani Aondolewa Taifa Stars
Marcos Alonso Afanyiwa Vipimo Kimya Kimya