Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea amesema anaungana na wote wenye msimamo wa kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Dkt Mwigulu Nchemba ajiuzulu.
Kubenea amesema hayo akidai kuwa Waziri Mwigulu hana haiba nzuri ya uongozi kwani anashindwa kutumia vizuri nafasi yake kama Waziri.
Ametoa Kauli hiyo kufuatia matamshi alioyatoa Mwigulu juu ya Chadema akidai kuwa wanahusika katika shambulio lililotokea na kupelekea kifo cha mwanafunzi wa chuo cha Usafirishaji cha NIT, Akwilina Akwiline.
Katika mkutano wake na wanahabari, Kubenea amesema kwamba moja ya kauli ya Mwigulu aliyoitoa ni ile iliyonukuliwa kwenye mtandao mmoja akihoji kwanini ajiuzulu wakati Chadema ndiyo wanahusika na mauaji? na kuongeza kwamba tangu waziri huyo alipokuwa Kiongozi wa juu ndani ya CCM hakuwahi kuwa na maadili ya kuizungumzia vyema Chadema kwani amekuwa akiihusisha na mambo ya kihalifu.
-
Video: Rais Magufuli asafiri nje ya nchi kushiriki mkutano wa wakuu wa nchi EAC
-
Lema atajwa kuwa chanzo cha madiwani kuhama chama
Pamoja na hayo, Kubenea amedai kwamba kama Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni angetoa vibali vya viapo vya Uchaguzi mapema, Chadema wasingeandamana na huu uchunguzi ungekua halali hayo yote yasingetokea