Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda jana aliamuru polisi kumkamata mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea baada ya kutofautiana wakati wa kuumaliza mgogoro kati ya uongozi na wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha TZ TOOKU.

Sakata hilo lilitokea jana baada ya mbunge huyo wa Ubungo kufika katika kiwanda hicho kwa lengo la kutatua mgogoro huo baada ya kupigiwa simu na wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Baada ya ‘vutankuvute’ ya muda getini na mlinzi, Kubenea alifanikiwa kuruhusiwa kuingia ndani na kuonana na uongozi wa kiwanda hicho na kufanya nao mazungumzo kwa takribani saa mbili akiwa na wawakilishi wa wafanyakazi.

Muda mfupi baada ya kumaliza kikao hicho, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda aliwasili. Baada ya mazungumzo ya muda, aliwaeleza wananchi hao kuwa leo atafika katika kiwanda hicho akiwa na mawaziri wa wizara husika ili kulitatua tatizo lao. Aliwataja mawaziri hao kuwa ni waziri wa Biashara na Viwanda, Waziri wa Kazi na Ajira pamoja na waziri wa Afya, Jinsia, Watoto na Wazee.

Hata hivyo, ziara hiyo iliingia doa baada ya kutokea mvutano kati ya mkuu huyo wa wilaya na mbunge wa Ubungo, ambapo mbunge alitaka kuzungumza na wafanyakazi kwa lengo la kuwaaga huku Mkuu wa Wilaya akitaka asitishe zoezi hilo na watu wote watawanyike.

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda Akizungumza na Mbunge wa Ubunge Saed Kubenea

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda Akizungumza na Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea

Katika hatua za mvutano, Makonda alidai kukosewa adabu na mbunge huyo kwa madai kuwa alimuita kibaka. Mvutano huo ulimalizika baada ya Makonda kuagiza polisi kumtia nguvuni Kubenea na kumpeleka katika kituo cha polisi cha Magomeni.

 

 

 

Mwana FA: Wasanii wa Tanzania Tunaukosea Adabu Muziki
Kasi Ya Magufuli Yampitia ‘Dk. Mwaka’, Atimua Mbio, Atakiwa Kujisalimisha