Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Saed Kubenea ameugua ghafla na kupumzishwa katika Zahanati ya Bunge baada ya kujisikia vibaya.

Kubenea leo alienda Mjini Dodoma kwa ajili ya kuripoti bungeni lakini kwa bahati mbaya alijisikia vibaya na kuelekea katika Zahanati ya Bunge ili apatiwe matibabu lakini ghafla hali ilibadilika hivyo kupelea kupumzishwa.

Hata hivyo, Kubenea amepumzishwa katika Hospitali ya bunge mjini Dodoma japo mpaka sasa bado haijafahamika nini hasa kinachomsumbua na kupelekea kutokea kwa hali hiyo iliyomkumba.

Serikali kuendelea kulijengea uwezo Bunge
Bunge latoa ufafanuzi kuhusu kauli ya Spika Ndugai