Katika harakati za kueleka uchaguzi mkuu nchini Kenya Agosti 2022, utafiti uliofanywa kwa kura ya maoni na kampuni ya TIFA unaonyesha kuwa naibu rais William Ruto ndiye maarufu zaidi katika kinyang’anyiro cha urais.

Majibu ya utafiti huo yaliyotolewa Alhamisi Februari 17, 2022 pia unasema Gavana Ann Waiguru na Peter Kenneth ndio wanapendelewa zaidi kama wagombea wenza wa Ruto na Raila kutoka Mt Kenya

Kulingana na utafiti huo, uchaguzi wa urais ukifanywa leo, DP Ruto atambwaga hasimu wake wa ODM Raila Odinga kwa uwa inaonesha RUTO anaongoza kwa asilimia 38 huku Raila akiwa wa pili na asilimia 27 wakiwa ndio wagombea wakuu kwenye mbio za kuingia Ikulu.

Aidha Musalia Mudavadi na Peter Kenneth nao ndio wanapendwa zaidi katika nyadhifa za wagombea wenza ndani ya Kenya Kwanza na Azimio la Umoja.

Utafiti mwingine uliofanywa na kampuni ta Radio Africa nao ulionyesha DP Ruto anaendelea kuongoza lakini umaarufu wake unapungua.

Raila naye amekuwa akiongeza umaarufu katika safari ya kutafuta mrithi wa Rais Kenyatta katika uchaguzi wa Agosti ikiwa kiongozi huyo wa ODM anatarajiwa kupigwa jeki baada ya Rais Uhuru kusema kuwa Jubilee itamuunga mkono.

Rais Uhuru Kenyatta mpaka sasa ameonesha msimamo wake ni kwa Raila kwa kuwa mara kadhaa ameshamuongelea kama mrithi wake na akisema kuwa chama chake kitatia nguvu katika kampeni za Raila na kuhakikisha anashinda.

EU warejesha mahusiano Tanzania
RC Makalla hakuna shule iliyouzwa Kurasini