Maduka ya Uchumi maarufu kama ‘Uchumi Supermarkets’ nchini Tanzania na Uganda yamefungwa rasmi baada ya kutoingiza faida kwa kipindi cha miaka 5.

Mkurungenzi Mkuu wa ‘Uchumi Supermarkets’, Dkt. Julius Kipng’etich amesema kuwa wamechukua maamuzi hayo kwa lengo la kutathmini muunda wa oparesheni zake nchini Kenya, kwa kuwa maduka hayo ya Tanzania na Uganda yamekuwa yakitegemea faida inayotengenezwa na maduka yaliyoko nchini Kenya.

“Maduka yetu nchini Tanzania na Uganda yanajumlisha asilimia 4.75 ya oparesheni zetu licha ya kutugharimu asilimia 25 ya oparesheni zetu,” alisema Dkt. Kipng’etich.

Hatua hiyo imetangazwa siku chache baada ya kuwepo taarifa kuwa wafanyakazi wa maduka hayo nchini Tanzania waliwabana waajiri wao wakidai kupata muafaka kabla ya maduka hayo kufungwa rasmi.

 

FA Yamuadhibu Tena Jose Mourinho
Lembeli Awapa Neno Wagombea Wa CCM Waliomtangazia ‘Maafa’ Baada Ya Ajali