Jimbo la Arusha Mjini limekamilisha zoezi la uchaguzi mdogo wa wabunge jana, Disemba 13 likiwa kati ya majimbo mengine yaliyofanya uchaguzi mdogo huku macho ya watu wengi yakielekezwa jimboni humo.

Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyokusanywa kwenye vituo 26 vya kupigia kura, mgombea ubunge wa Chadema, Godbless Lema anaonekana kuongoza na kuna dalili kubwa za kupata ushindi wa kishindo dhidi ya mshindani wake mkuu, Philemon Mollel  wa CCM.

Uchaguzi wa Arusha uliahirishwa kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea ubunge wa ACT-Wazalendo, Estomih Malla.

Hata hivyo, Msimamizi wa uchaguzi huo, Juma Idd alisema kuwa idadi ndogo sana ya wapiga kura ilijitokeza ukilinganisha na waliojiandikisha na kwamba muamko haukuwa sawa na ule wa Oktoba 25. “Hakuna hata foleni ya watu 10 wanaopanga kupiga kura, wanakuja mtu mmoja mmoja katika vituo vingi,” alisema Idd wakati zoezi hilo likiendelea jana.

Katika hatua nyingine, CCM imeonekana kuongoza katika majimbno mengine manne ya uchaguzi likiwemo jimbo la Handeni, Lushoto, Handeni Mjini na Lulindi.

Aliyekosoa chama tawala Kufungwa Jela Miaka Nane
Makaburi Kuwekewa Huduma ya Mtandao ya Wi-Fi