Kwa mujibu wa utafiti, uliochapishwa na Jarida la Kilimo na kemia la vyakula protini inayotokana na tunda la boga pr-2, husaidia kupambana na ugonjwa unaosababisha fangasi sehemu za siri kwa mwanamke.
Protini hiyo ya pr-2iliyopo katika maboga hutibu pia michubuko inayotokana na mkojo au nepi huku ikizuaia aina 10 za fangasi, ikiwemo candida albicans, fangasi ambayo ni maarufu kwa kusababisha matatizo kwa watu wenye kisukari katika ngozi, chini ya kucha na katika mfumo mzima wa mwili.
Hata hivyo, wataalamu wa maswala ya lishe wanasema kuwa gram moja ya mbegu za maboga na mbegu zina vitamini sawa na glasi moja ya maziwa, hivyo ni wajibu wa kula wa kula maboga na mbegu zake kwaajili ya kupata vitamini hiyo.
Mtaalamu wa lishe utoka TFNC Elizabeth Lyimo amesema kuwa boga lina protini ambayo husaidia kupambana na magonjwa yatokanayo na fangasi na kuongeza kuwa mbegu zake pia zimesheheni protini, madini ya chuma, kopa, maginiziam, na zink.
”Licha ya kusheheni madini na protini hizo bado baadhi yetu hatujui faida ya boga mwilini pia Juisi ya boga lililochemshwa ni nzuri ni nzuri kwa wtoto wa miezi sita na kuendelea, katika mlo wa mtoto jaribu jaribu kumsagia kiasi kidogo cha boga lilochemshwa vizuri angalau mara moja kwa siku” amesema Elizabeth.
Aidha, amesema mbegu za maboga huimarisha kinga za mwili na ukuaji wa seli lakini pia kwa wale wanaokosa usingizi hawana budi kutumia mbegu za maboga pale wanapotaka kulala na maboga yamekuwa yakitumika katika tiba za kiasili kwa nchi za China, Korea, India, Yugoslavia, Argentina, Mexico na Brazil.