Hakuna kitu kizuri kama kuwa na nwyele zenye muonekano mzuri, imara na zakuvutia haijalishi ni ndefu au fupi lakini kila unapo peleka mkono wako kichwani unapata hisia zakuendelea kuzishika, hali hii ni kwajinsia zote wanawake na wanaume.
Lakini jambo hili sio rahisi kufanikisha kwani kwa muda mrefu sasa watu wengi wamekuwa wakihangaika bila mafanikio na wengine kujikuta wanaishia kunyoa vipara au kuvumilia kuwa na muonekano wa nywele zisizo vutia, leo utafahumu aina za vyakula ambavyo vinahusika moja kwa moja na ustawi wa nywele zako.
Utafiti uliofanywa na shirika lisilo la kiserikali la nchini Marekani ” American Hair Loss association” linaloshughulika na masula ya ukuaji wa nywele, matatizo yake na matibabu yakiwepo asilia, hivi ndiyo vyakula vitano unavyoweza kula na kuokoa nywele zako.
- Mboga za Majani
Unaweza kuwa umesha shauriwa mara kadhaa kula mboga za majani na uka puuza , basi kama unahitaji nywelezako zikue na ziwe na afya kula mboga za majani kwa wingi kama mchicha, spinach na figiri kwani zina madi ya chuma ambayo yana hitajika sana katika ukuaji wako wa nywele.
Utafiti unaonesha kuwa madini ya chuma yanasaidia sana nywele kukua vizuri na kuto nyonyoka hii kwasababu chuma ni ishara tosha yakuwa hewa ya Oxygen na virutubisho vyote havitoki kwenye vijitundu vya nywele , hivyo kupelekea mjongeo imara wa nywele zako.
2. Matunda jamii ya Michungwa
Haya unaweza ukayala yenyewe kama matunda au kajijengea mazoea yakunywa juice yake, sio lazima ule yote kwa pamoja unaweza ukapanga ratiba nzuri.
Matunda haya yanasifika sana kwakuwa na vitamin C ambayo inamchango mkubwa katika ukuaji wa nywele kwani utafiti unaonesha kuwa vitamin C inafanya kazi vizuri na madini ya chuma kukuza nywele.
Matunda hayo ni kama Machungwa yenyewe, Limao, Ndim, na mapingiles, ambayo pia huzalisha Collagen inayokuza nywele na kuifanya imara kuanzia chini hadi juu kwenye ncha.
3. Viazi vitamu
Watu wengi hudhani kuwa moja ya kiungo cha mwili ambacho hukuwa kwa tratibu zaidi ni nywele, lahasha hii siyo kweli nywele ndiyo kiungo kinachokuwa kwa uharaka zaidi katika mwili wa binadamu kwasabau ngozi ya kichwa huzalisha tissue kwa uharaka zaidi lakini katika hilo ili ngozi hiyo izalishe tissue inahitaji Vitamin A.
Viazi hivi vina utajiri mkubwa sana wa Vitamin A, ambayo vimegawanyika katika makundi mbalimbali, vipo vyeupe, vyanjano na viazi lishe lakini vyote vina vitamin A, na inashauriwa kula kidogokigogo hadi mara nne kwa siku yani kwakila mlo uwe na kiazi kidogo kitam.
4. Mayai
Protini ni muhimu sana katika ukuaji wa nywele imara na kuhakikisha nywele zinz afya, hii ni kwasababu nywele pia zimeunda kwa protini yani zinzprotini ndani yake.
Hivyo basi kumujibu wa utafiti uliofanywa imeshauriwa kuwa ulaji mayai unasaidia sana kukua kwa nywele kwani unaongeza kiasi cha protini kwenye nywele .
Hata hivyo utafiti unaonesha kuwa mayai yana protini nyingi sana kwani katika kila yai moja kuna gram 6 – 7 za protini ambazo zitasaidia ukuaji wa nywele zako.
5. Parachichi
Tunda hili wingi hutumia kwa kupaka kwenye nywele lakini jambo la muhimu la kufahamu ni kwamba unapo kula linafanyakazi maradufu ya kupaka kichwani.
Kwamujibu wa tafiti za kisayansi tunda hili ni latofauti na la aina yake kwani lina Vitamin A,D,E, na B6 na madini ya Magnesium, Protini madini chuma na mengine mengi, ambapo licha ya kuwa na umuhimu katika mwili wa binadamu, Vitamini E vilivyopo ndaniyake husaidia kutengeneza mzunguko mzuri wa damu ambao unahitajika sana katika ukuaji wa nywele.
Kwahiyo kama unakula mboga zamajani, machungwa, mayai, viazi vitamu chakula cha mwisho muhimu au tunda ni Parachichi ambalo unaweza kula kama tunda au ukasaga juice yake ambayo ina radha nzuri pia.