Imefahamika kuwa ushindi wa mabao 2-0 walioupata Young Africans dhidi ya Al Merreikh kwenye Ligi ya Mabingwa juzi Jumamosi (Septemba 16) haukuja hivi hivi kwa kuwa nyuma ya pazia Rais wa klabu hiyo Injinia Hersi Said alimwaga fedha za maana.

Taarifa rasmi kutoka kwa uongozi wa Young Africans umeweka wazi kuwa Rais huyo alitumia zaidi ya shilingi milioni 40 kununua tiketi kwa ajili ya mashabiki hao ambao walikuwa sehemu ya historia ya Young Africans.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alithibitisha juu ya hilo kwa kusema: “Rais wetu Injinia Hersi Said alitoa zaidi ya shilingi milioni 40 kwa ajili ya mashabiki wake kuingia uwanjani, hiyo ni zaidi ya upendo kwa Rais wetu kwani ingekuwa rahisi kwake kwenda kutumia hizo pesa katika mambo yake mengine.

“Lakini badala yake ameamua kuonyesha upendo mkubwa kwa mashabiki wa timu hii, hii ndio maana halisi ya timu ya Wananchi kwa kuwa umoja na kushikamana, tuwashukuru mashabiki wote wa Young Africans ambao walikwenda Rwanda kuisapoti timu na tumepata ushindi kwa ajili yao,’ amesema Kamwe.

Mbaazi zawapa Wakulima tabasamu la Bil. 32.8
Joao FĂ©lix: Ninafurahia maisha FC Barcelona