Siri ya klabu ya Liverpool kuegemea sana kwa meneja wa kijerumani Jurgen Klopp na kuachana na aliyekua meneja wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti, imefichuka ikiwa ni siku mbili zimepita baada ya uongozi wa klabu hiyo ya Anfield kuanza mchakato wa kumsaka mbadala wa Brendan Rodgers aliyeonyeshwa mlango wa kutokea mwishoni mwa juma lililopita.

Uchunguzi uliofanywa na kituo cha televisheni cha Sky Sports cha nchini England umeibini, Liverpool walikua na shauku ya kutaka kumpa ajira Carlo Ancelotti, lakini walikutana na changamoto kubwa.

Watu wa karibu wa meneja huyo kutoka nchini Italia wameeleza kwamba, Liverpool walianza kufanya mawasiliano na Ancelotti kwa kumtaka achukue nafasi iliyoachwa wazi na Rodgers, lakini alikataa kuitimia wito huo.

Watu hao wametanabaisha kwamba, Ancelotti ameendelea kusimamia maamuzi ya kutaka kuwa pembeni na soka katika msimu huu, na amejipanga kurejea tena kazini msimu ujao.

Msimamo wa Ancelotti, ulitoa nafasi kwa viongozi wa klabu ya klabu ya Liverpool kuanza mchakato wa kumshawishi aliyekua meneja wa klabu ya Borussia Dortmund, Jurgen Klopp, ambaye kwa sasa inasemekana yupo njiani kuelekea Anfield.

Ancelotti, mwenye umri wa miaka 56, aliwahi kufanya kazi nchini England akiwa na klabu ya Chelsea kuanzia mwaka 2009-11 na alifanikiwa kutwaa ubingwa wa nchini humo pamoja na kombe la FA msimu wa 2009-10 na mwaka 2009 aliiwezesha The Blues kuchukua ngao ya jamii.

Watendaji Wa Tanesco Kufutwa Kazi Na Rais Huyu Wa Awamu Ya Tano
Magufuli Atua Kwa Lowassa, Amwaga Ahadi