Mshambuliaji kutika DR Congo na klabu ya AS Vita Club Fiston Mayele inadaiwa tayari amemalizana na Kocha Nasreddine Nabi na anachosubiria sasa ni viongozi wa Young Africans kumleta Dar es salaam, Tanzania.

Mayele akiwa na AS Vita msimu uliopita alitupia mabao 13 na kuwa mfungaji namba mbili kwenye ligi ngumu ya DR Congo amefunguka kwamba, tayari amehakikishiwa nafasi na kocha huyo kwenye kikosi cha Young Africans msimu ujao wa 2021-22.

“Kocha Nabi ameniambia anataka nije Young Africans nimeongea naye sana na kwa sasa nasubiri simu ya viongozi wao tumalizie mpango wa usajili,”

“Sina wasiwasi na kazi yangu. Najua kufunga. Hapo kuna viungo wazuri sana ambao tukisaidiana kwa pamoja ni rahisi kufanikiwa. Nafurahi pia kuwa timu itakuwa inashiriki mashindano ya Afrika.” amesema Fiston Mayele.

Young Afrcans wanaendelea kujizatiti kwenye maboresho wa kikosi chao kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa msimu ujao.

Tayari inadaiwa wameshaamalizana na Beki wa Pembeni wa AS Vita Club Djuma Shaaban na Kiungo fundi wa Dodoma Jiji Dickson Ambundo.

Nabi: Naiheshimu sana Simba SC
Samatta kuvaa jezi namba 15