Aliyewahi kuwa kocha Mkuu wa Real Madrid Zinedine Zidane ameripotiwa alikubali kurejea katika kazi ya ukocha lakini kwa sharti moja tu!
Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa ana ushawishi mkubwa kwenye ulimwengu wa soka akiwa kama kocha licha ya kustaafu, alionyesha nia ya kuinoa moja ya timu kutoka Ufaransa.
Zidane aliiongoza Madrid kunyakua mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa akiwa kama kocha mkuu, pia aliipa UEFA Super Cup na Kombe la Dunia la klabu la FIFA mara mbili, pamoja na taji la La Liga na Supercopa.
Hata hivyo, mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 51 hajawahi kufundisha nje ya Hispania na nafasi yake ya mwisho akiwa kocha wa Madrid ilikuwa kuanzia mwaka 2019 hadi 2021.
Sasa iliripotiwa Mfaransa huyo aliamua kurudi upya huku akihusishwa na klabu ya Olympique de Marseille ya Ufaransa.
Ripoti hiyo inasema Zidane alikubali kuwa kocha wa Marseille hata hivyo, kuna sharti moja ambalo lazima litimizwe endapo angeteuliwa.
Inasemekana alikubali kuwa meneja mpya wa Marseille endapo klabu hiyo itauzwa kwa mwekezaji kutoka Saudi Arabia.
Lakini sharti la Zidane lingekuwa gumu kutimizwa kwani mmiliki wa sasa Frank MeCourt, ambaye alinunua klabu hiyo miaka saba tu iliyopita, alisisitiza katika miezi ya hivi karibuni kwamba hana mpango wa kuipiga bei.