Meya wa jiji la Dar es Salaam Omari Kumbilamoto amesema serikali imefikia muafaka wa kutatua changamoto inayowakabili wananchi hasa wanafunzi wa kata ya Ukonga na maeneo ya karibu kwa kuwajengea shule ya sekondari iliyokuwa ikisuasua kutokana na ufinyu wa eneo.

Ameyasema hayo mapema leo wakati akikabidhi msaada wa magodoro 42 yenye thamani ya takribani milioni 1.5 kwa wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya msingi Ukonga

Amesema kuwa idadi kubwa ya wanafunzi hao wenye ulemavu wa kusikia wanakaa mbali na wamekuwa wakipata shida kutoka nyumbani hadi shuleni.

“Mabweni tulisha yakamilisha lakini changamoto ilikuwa ni magodoro lakini leo tumeweza kuyakabidhi, pia nimshukuru Mkurugenzi wa Mamlaka ya Anga TCAA, Hamza Johari ameweza kutujengea matundu ya vyoo 10 yenye thamani ya milioni 16 katika shule hii,” amesema Kumbilamoto

Halikadhalika amesema changamoto wanafunzi hao wanayokutana nayo serikali iliwajengea mabweni na kuwapatia msaada wa magodoro ili kuwawezesha kukaa mazingira ya karibu na shule.

RC Makalla awapa matumaini mapya wafanyabiashara soko la machinga complex
Uelewa wa sheria wageuka 'janga'