Rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amani Karume ni mmoja wa waasisi taifa, aliongoza Zanzibar baada ya mapinduzi yaliyomuangusha Sultani aliyekuwa akitawala visiwa hivyo.
Mwaka 1964 mwanzoni baada ya mapinduzi hayo Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa inaongozwa na mwalimu Julius Nyerere na kuzaliwa Tanzania.
Karume alipatwa na umauti baada ya kupigwa risasi visiwani humo April 7, 1972 akiwa na miaka 67, katika ofisi za makao makuu ya CCM eneo la Kisiwandui visiwani Zanzibar.
Historia inaeleza kuwa alipigwa risasi wakati akicheza mchezo wa bao na wenzake, ambapo aliyemuua naye aliuawa papo hapo na walinzi wa Karume, baada ya kutokea kwa tukio hilo.
Hata hivyo Mzee Karume alikuwa makamu wa Rais wa kwanza wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Rais ambapo Karume alitawala Zanzibar kwa miaka minne.