Nahodha na Mshambuliaji wa FC Barcelona pamoja na Timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi amesema kwa sasa ni mchezaji huru na anaweza kuondoka ndani ya klabu hiyo.

Messi amesema anaamini kwa sasa ni mchezaji huru na anaweza kwenda kujiunga na klabu yoyote. Hilo ni tofauti na Barcelona ambao kwa upande wao wanadai bado ana mwaka mmoja na akiwa na ‘release clause’ ya paundi milioni 629.

Iwapo Man City itaamini maneno hayo ya Messi ni sahihi kuwa yupo huru italazimika kupata ‘provisional international transfer certificate (ITC) kutoka Shirikisho la Soka Duniani FIFA na kumsajili ili kuanza kuwatumikia msimu wa 2020/21 utakaoanza mwezi Septemba.

Mpaka sasa Shirikisho la Soka Duniani FIFA ndilo lenye uwezo wa kuamua mzozo utakaojitokeza kati ya Barcelona na Manchester City inayotaka kumsajili Messi kwa ajili ya msimu ujao.

Endapo FIFA itasema Messi yupo sahihi kuwa ni mchezaji huru basi moja kwa moja atajiunga na Man City. Lakini kama FIFA itasema Barcelona ndiyo ipo sahihi basi City italazimika kutoa ‘release clause’ kama inamuhitaji.

Mkataba wa mwisho Messi aliyoanguka saini mwaka 2017 ulimpa ruksa ya kuondoka bure kila ifikapo mwisho wa msimu kama atahitaji kufanya hivyo na kutoa taarifa mapema katika siku 10 za kwanza za mwezi Juni.

Lakini endapo hakutakuwa na taarifa zozote kutoka kwa Messi za kuomba kuondoka baada ya kupita siku 10 za mwanzo za mwezi Juni, klabu itachukulia kuwa dirisha hilo limepita kwa maana hiyo atakuwa na mwaka mwengine ndani ya timu.

Messi anatafsiri tofauti, kama mkataba unamruhusu kuondoka kama mchezaji huru kila mwishoni wa msimu, na msimu huu haukuisha hadi mwezi Agosti, hivyo anaamini anaweza kwenda pasipo malipo.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, agosti 28, 2020
Polisi Dodoma wajipanga kuelekea Uchaguzi Mkuu