Kundi linaloaminiwa kuwa ni la waasi wa The Allied Democratic Forces (ADF), limewaua watu 12 katika mji wa mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na meya wa mji huo, Modeste Bakwanamaha alipo thibitisha kutokea kwa mauaji hayo ya wananchi wasio na hatia wa eneo lake amesema kuwa mauaji hayo yamekuwa yakishuhudiwa tangu siku ya jumatatu juni 03.
Ripoti zilizotolewa zinasema kuwa waasi hao walitekeleza mashambulizi mengine pia katika kambi ya jeshi ya Rwangoma na kuua wanajeshi wawili lakini baada ya kuzidiwa nguvu na wanajeshi hao walikimbia.
Ikumbukwe kuwa tangu mwaka 2014, makundi ya waasi wamekuwa wakishambuliwa katika makazi hayo ya mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya congo suala ambalo limepelekea wananchi wa eneo hilo kushinikiza serikali kuongeza juhudi za kuimarisha usalama.