Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge leo Mei 26, 2021 ameendesha Kikao cha wadau wa zao la Ufuta mkoani hapo ili kujua changamoto za wakulima wao.

Akizungumza katika kikao hicho kiliochofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha FDC-Ikwiriri Wilayani Rufiji, unenge ameonesha kukerwa na madhaifu ya kiutendaji, urasimu, ucheleweshaji wa pembejeo, vifungashio na kuchelewa kuanza kwa mnada wa kwanza.

Kunenge amewataka wakulima kulima kwa tija na kuwaahidi kuwa Serikali ipo tayari kuwasaidia ili waweze kuzalisha kwa tija.

Aidha, Kunenge ameagiza wataalamu wa ofisi yake kufanya tathimini ya zao hilo na kuja na mkakati maalum utakaosaidia kukuza zao hilo.

Tanzania yapewa mkopo wa Bilioni 323
Kumbukumbu ya Hayati Sokoine yampeleka Dkt. Mpango Morogoro