Waziri wa Elimu wa Ufaransa, Gabriel Attal amesema Serikali imelazimika kuzifunga Shule saba zenye Wanafunzi wapatao 1,500 baada ya kuvamiwa na kunguni, ikiwa ni tukio la pili baada ya mapema wiki hii pia kutangazwa kufungwa kwa Shule mbili kwa sababu kama hiyo ikiwemo ile Marseille na nyingine Villefranche-sur-Saone zilizopo nje kidogo ya mji wa kusini mashariki wa Lyon.

Attal ameyasema hayo Oktoba 6, 2023 na kusema Serikali imeanza kuchunguza idadi inayoongezeka ya visa vya kunguni, wakati nchi hiyo ikiandaa Kombe la Dunia la Rugby na ambayo itakuwa mwenyeji ya Michezo ya Olimpiki 2023 huku Waziri Mkuu, Elisabeth Borne akiitisha kikao cha Baraza la Mawaziri kujadili namna ya kupambana na kunguni.

Kwa upande wake Waziri wa Usafiri, Clement Beaune alikutana wiki hii na makampuni ya usafirishaji kubuni mpango wa kufuatilia na kunyunyizia dawa vyombo vya usafiri wa umma na, yumkini, kujaribu kupunguza wasiwasi wa nchi nzima uliochochewa zaidi na vyombo vya habari.

Hata hivyo, baada ya taarifa kuwa kunguni walipatikana kwenye jengo la sinema mwezi mmoja uliopita, raia wa Ufaransa walianza kusambaza video katika mitandao ya kijamii zikionesha wadudu hao wakitambaa majumbani na kwenye usafiri wa umma kama matreni na mabasi.

Takwimu za Shirika la Afya na Usalama wa Chakula nchini Ufaransa, zinaonesha nyumba moja kati ya kumi nchini humo ilikuwa na kunguni katika miaka michache iliyopita huku ikiarifiwa kuwa ili kuwatokomeza kunguni itagharimu pesa nyingi na zoezi hilo si la mara moja.

Mbunge Mwangachuchu ahukumiwa kifo kwa uhaini
Klopp: Dunia imenielewa tofauti