Ofisi ya Waziri Mkuu nchini Israel, imesema muungano unaotawala utapiga kura ya kulivunja Bunge kabla ya mwisho wa mwezi huu, na kupelekea nchi hiyo kuingi katika uchaguzi wake wa tano katika kipindi cha miaka mitatu.

Hatua hiyo, inatokana na kuasi kwa wabunge wawili wa mrengo wa kulia na uasi wa mara kwa mara wa wengine watatu, na kufanya muungano wa Waziri Mkuu Naftali Bennett kutokuwa wengi katika Bunge.

Kuanguka huko kunatoa mkondo wa kisiasa kwa Waziri Mkuu wa zamani Benjamin Netanyahu, ambaye aliondoka madarakani Juni mwaka jana 2020 na ambaye chama chake cha Likud kinaongoza kwa sasa katika kura za maoni.

Hata hivyo, uchaguzi huo unaotazamiwa kufanyika mwishoni mwa msimu huu, unakuja katika wakati mgumu baada ya kuongezeka kwa mashambulizi ya Wapalestina dhidi ya Waisraeli na kuongezeka kwa vita vya kivuli kati ya Israel na Iran.

Mkataba wa sasa wa muungano unamtaka Yair Lapid, Waziri wa Mambo ya nje na mtangazaji mkuu wa zamani, achukue nafasi ya Waziri Mkuu wa mpito katika tukio ambalo uasi wa mrengo wa kulia utasababisha uchaguzi wa mapema.

Inadaiwa kuwa endapo makubaliano hayo yataheshimiwa, Lapid ataongoza Serikali kwa miezi kadhaa.

Victor Akpan aipotezea Simba SC
Simba SC yakanusha uvumi wa Bernard Morrison