Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa amesikitishwa na vitendo vya Mabalozi kushindwa kutekeleza maagizo yake aliyowapa ya kumpa taarifa juu ya utendaji kazi wao na manufaa ambayo Tanzania imeyapata kwa uwepo wa kila Balozi katika nchi aliyopangiwa kila robo mwaka.
Ameyasema hayo Ikulu Jijini Dar es salaam mara baada ya kumaliza kumuapisha, Alphayo Kidata kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada na Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora.
Amewataka viongozi hao kwenda kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kwa manufaa ya Taifa na sio kufanya mambo ndivyo sivyo.
“Balozi ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika nchi fulani, nchi imenufaikaje na uwepo wake kwenye nchi ile?. Kuteuliwa sawa lakini sio lazima ukae katika ubalozi huo kwa kipindi chote ulichopangiwa, ukishindwa kuleta manufaa unarudishwa na huko anapangiwa mtu mwingine atakayeleta manufaa kwa nchi,”amesema Rais Dkt. Magufuli
-
Serikali yazindua chanjo ya kudhibiti Ukimwi kwa 90%
-
Heche akerwa na serikali ya CCM aitaka iwe sikivu
-
Sababu ya Sugu kuachiwa huru yaanikwa
Hata hivyo,Rais Dkt. Magufuli ameipongeza Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kufanya kazi nzuri katika sekta ya Elimu na Afya