Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demnokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Tundu Lissu amesema kuwa mpinzani au uwepo wa suala la kupingana sio kosa la jinai kwani watu hutofautiana kiitikadi na hata katika utekelezaji wa mambo mbalimbali yenye kuleta maendeleo kwa jamii.
Lissu ameyasema hayo wakati akifanya Mahojiano maalum na Dar24 Media nyumbani kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kudai kuwa viongozi wengi wa CHADEMMA wakemuwa wakikamatwa kwa kubambikiwa makosa ambayo siyo ya kweli, na hilo linafahamika na Viongozi wa Kitaifa.
Amesema, “Tulimwambia Rais Samia kukutana kwetu hakuna maana kama watu wetu, Viongozi wetu wanaendelea kushikiliwa na vyombo vya jinai kwa makosa ambayo siyo ya kweli, na hata yeye tulimwambia kwamba anajua makosa ni ya kubambikiwa si ya kweli, ujue kuwa mpinzani sio kosa la jinai.”
Aidha Lissu ameongeza kuwa, wakati alipokutana na Rais Samia Brussels nchini Ubelgiji Februari 17, 2022 alimuambia kuwa wao na Dunia hawamuelewi na hawatamuelewa iwapo anahubiri upendo wakati Mwenyekiti wa upinzani yupo Gerezani kwa kesi ya ugaidi wa uongo, na Rais Samia aliahidi kuwaachilia huru.