Nahodha wa timu ya Borussia Dortmund Marco Reus, amefurahia mpango wa klabu hiyo wa kuendelea kufanya kazi na kiungo kutoka England Jadon Sancho, licha ya tetesi kueleza kuwa Manchester United wanajipanga kumsajili katika kipindi hiki cha usajili.

Manchester United walijaribu zaidi ya mara moja kuwasilisha ofa ya kumsajili kiungo huyo ili kuimarisha nguvu ya kikosi chao lakini walikwama kufuatia uongozi wa Dortmund kuhitaji Euro milioni 120 sawa na Pauni milioni 108, kama ada ya usajili wa Sancho.

Sancho bado ana makataba na klabu hiyo ya Ujerumani hadi mwaka 2023 na Reus amefurahishwa kuendelea kucheza pamoja na mchezaji huyo wa zamani wa kikosi cha vijana cha Manchester City.

“Kwetu ni jambo kubwa, tunafuraha kwamba tutaendelea kuwa naye walau mwaka mmoja, ndiyo kwa sababu bado anaendelea na kasi yake ya kutengeza usaidizi wa kupatikana mabao na kusumbua ngome ya upinzani tutapata alama nyingi.” Amesema Reus

Hata hivyo nahodha huyo wa BVB hakuwa tayari kumfananisha Sancho na wachezaji wengine kama Lionel Messi na Christiano Ronaldo, zaidi ya kumsifia kwa kusema: “Ni mchezaji mzuri sana katika timu yetu na huenda siku moja atakuja kuwa mchezaji mkubwa kama wachezaji wawili (Messi na Ronaldo) tutaona.

“Anahitaji muda na uzoefu lakini pia kuna wakati mambo huwa hayaendi poa lakini akiwekeza bidii na kujituma atafika sababu anakipaji kikubwa.

Sancho alifunga mabao 17 msimu uliopita nyuma ya Thomas Muller (21), Timo Werner (28) na Robert Lewandowski (34) na kuwa ni mchezaji pekee aliyetoa pasi za mwisho 16 katika Ligi ya Ujerumani (Bundesliga).

Dortmund itawakabili Bayern Munich katika michuano ya German Super Cup siku ya leso usiku, huku wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa mabao mawili kwa sifuri na Augsburg katika Bundesliga siku ya Jumamosi.

Tetesi: Toreira kutua Atletico Madrid
Lissu : Itabidi tubadilishe katiba kwanza