Maafisa wa ngazi za juu toka Israel na marekani wamewasili Umoja wa Falme za Kiarabu , kupitia ndege ya kwanza ya kibiashara toka mataifa ya mashariki ya kati ikiwa ni kuweka shinikizo la mahusiano mazuri na ya wazi baina ya mataifa hayo .
Ndege namba LY971 ikiwa imepapwa kwa rangi za bendera ya Israel iliruka moja kwa moja toka Tel Aviv na kutua jiji la Abu Dhabi mji mkuu wa Falme za kiarabu imewasili ikiwa na Wasaidizi wakuu wa rais Donald Trump na waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.
Pia kwa mara ya kwanza ndege hiyo ,siku ya jumapili Agosti 30 ilipata kuruka katika anga la nchi ya Saudi Arabia baada ya makubaliano kuanza.
Ndege hiyo iliyobeba viongozi wan chi hizo mbili imechapishwa neno “Amani” kwa lugha ya kingereza, kiibrania pamoja na kiarabu. Pia denge hiyo imepewa jina la Kiryat Gat,ikimaanisha makazi ya Wayahudi huko Palestina, Iraq al-Manshiyya na al-Faluja
Agosti 13 ilitangazwa mwanzo wa kuhalalisha ushirikiano wa kimaeneo na makazi kati ya nchi za kiarabu na Israel ambao kwa kiasi miaka 20 umekuwa ukichochewa hofu toka kwa taifa la Irani
Wapalestina walishutushwa na hatua ya umoja wa Falme za Ki arabu , hofu ya muda mrefu ingeweza kudhoofisha msimamo wa kiarabu juu ya sakata hili .