Rais wa Urusi, Vladimir Putin amewasili nchini China kukutana na rafiki wake mkuu Rais Xi Jinping katika ziara inayolenga kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili wakitarajia kufanya mazungumzo pembezoni mwa Mkutano.

China wiki hii inatarajiwa kuwa mwenyeji wawakilishi kutoka katika mataifa 130 ya dunia, katika kongamano rais Xi kuhusu biashara na miundo mbinu na masuala ya barabara, linalofanyika wakati huu mapigano yakiendelea kuripotiwa kati ya Wanajeshi wa Israeli na wapiganaji wa Hamas.

Rais Putin ni miongoni mwa wageni wa ngazi ya juu kwenye kongamano hilo, hii ikiwa ni ziara yake ya kwanza kwenye taifa lenye uchumi mkubwa tangu nchi yake kuivamia Ukraine, kitendo ambacho kiliifanya kutengwa na baadhi ya mataifa ya Dunia.

Hata hivyo, Kremlin imesema suala la Israeli na Hamas pia litapewa nafasi katika kongamano hilo ambapo Mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani yameonekana kuunga mkono Israeli tangu Hamas kutekeleza shambulizi mbaya zaidi katika historia dhidi yake.

Habari Kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 18, 2023
Serikali yaendeleza sera mfumo jumuishi Uchumi wa Buluu