Katika kikao cha bunge la 1O, moja ya mijadala iliyoibuliwa ni swala zima la ufaulu mbovu kwa shule za Serikali ambapo wabunge wengi walihoji wizara ya Elimu.
Elimu ni sekta nyeti sana na ndio urithi pekee wa kudumu ambao wazazi wanatakiwa kuwarithisha vizazi vyao, lakini elimu ya Tanzania bado haijafikia kiwango cha kuridhisha.
Viongozi wanahoji kwa nini shule nyingi za serikali zinaufaulu mbovu kulinganisha na shule binafsi, majibu yapo wazi, shule binafsi zipo kibiashara zaidi na ili biashara ikae vizuri ipate wateja lazima iwe imejitosheleza kwa namna zote, ili kuvutia wateja, silaha kubwa kwa shule binafsi ni ufaulu mzuri.
Hali kadhalika shule nyingi za serikali zinakumbana na changamoto nyingi sana, ambazo kwa namna moja au nyingine ndio sababu kubwa ya wanafunzi kufeli, nashangaa kuona serikali inahoji kwa nini shule hizo zinafeli huku, miundombinu mibovu, mazingira mabaya ya walimu, wanafunzi wengi, walimu wachache na changamoto nyingine nyingi.
Zipo changamoto nyingi sana ambazo zitaichukua muda serikali kuhakikisha ufaulu wa shule binafsi unakwenda sambamba na ule wa serikali.
Ukizingatia sasa ni Elimu bure, hivyo wanafunzi wengi wamejazana shuleni ambako walimu ni wachache, kuna baadhi ya shule mwalimu mmoja anafundisha kidato cha kwanza hadi cha sita, huyo huyo atunge mitihani huyo huyo asahihishe kwahiyo utendaji kazi wa uyu mwalimu lazima utakuwa hafifu sio sawa na shule binafsi ambapo mwalimu mmoja anahudumia darasa moja lenye wanafunzi 40 tu.
Hivyo tunamwomba Rais Magufuli, kama alivyotangaza elimu bure basi asambaze na walimu mashuleni, kuna baadhi ya shule walimu walitumbuliwa kwa vyeti feki lakini hadi leo shule hizo hazijapatiwa walimu.
Na swala la uajiri wa wawalimu liende sambamba na uboreshwaji maisha ya walimu hao katika maeneo yao ya kazi.