Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amekemea tabia ya wakuu wa wilaya na mikoa kugombana wakati wanapotumikia wananchi.

Ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi wa wilaya ya Tarime mkoani Mara wakati wa ziara yake ya kikazi, ambapo kuna mgogoro mkubwa kati ya DC wa wilaya Glorius Luoga na mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Daud Ngicho na mkuu wa mkoa huo Adam Malima.

Rais Dkt. Magufuli ameonyesha kukerwa na misiguano ya viongozi wa mkoa wa Mara unaofanya hata miradi mbalimbali ya maendeleo kukwama kufuatia DC Luoga na RC Malima kutofautiana.

“Kwanini mnagombana, wewe DC uko chini ya RC Malima, umheshimu na si kugombana kila wakati mpaka shughuli za maendeleo zinakwama,”amesema JPM

Hata hivyo, hivi karibuni alikemea mgogoro kati ya mkuu wa wilaya ya Chemba na Naibu waziri wa Fedha, Dkt. Ashatu Kijaji na viongozi wa wilaya hiyo wakati wa kuzindua barabara inayounganisha Afrika.

 

 

Bobi Wine akutana na mbunge Marekani, amtaka Trump 'kuipotezea' Uganda
Rais Magufuli amepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa hii