Tangawizi ni kiungo kinachotokana na mizizi ya mmea wa tangawizi, Mmea huu unafanana na binzari ikiwa bado haijamenywa maganda yake. Kwa hapa Tanzania, hulimwa zaidi katika mikoa ya nyanda za juu kusini na baadhi ya mikoa kama Kilimanjaro, baadhi ya maeneo ya mkoa wa Manyara, Morogoro na kwingineko.

Mmea huu unaweza kuonekana kama wa kawaida na watu kuutumia tu kama mazoea, lakini kiungo hiki kinaweza kutumiwa kama dawa. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kimekaushwa na kutengenezwa unga.

Faida ya tangawizi huondoa arufu mbaya ya kinywa, kupunguza kichefuchefu, Husaidia msukumo wa damu mwilini kwasababu huupa joto mwili ambalo mara nyingi huitajika wakati wa usukumwaji wa damu mwilini.

Husaidia kuweka sawa kiwango cha sukari kwenye damu, husaidia mwili kunyonya virutubisho kwenye chakula, hupunguza mafuta kuganda kwa mafuta mwilini ambayo yana madhara mwilini.

Unywaji wa tangawizi husaidia uzalishaji wa mate mdomoni, kuongezeka kwa mate mdomoni husaidia kutengeneza vichocheo muhimu vinavyosaidia wakati wa kula na hupunguza pia uwezekano wa magojnwa ya meno.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 3, 2020
Waziri mkuu kuunda serikali ndani ya wiki mbili - Lebanon

Comments

comments