Mlinzi mpya wa Simba raia wa Ghana Asante Kwasi jana amefanikiwa kufunga bao katika mchezo wake wa kwanza na klabu yake hiyo mpya kwenye michuano ya Mapinduzi na kuwazidi mabao baadhi ya washambuliaji msimu huu.

Asante Kwasi ambaye amesajiliwa na Simba kwenye dirisha dogo akitokea Lipuli FC amekuwa miongoni mwa walinzi wenye uwezo mkubwa wa kufunga.

Aidha, akiwa na Lipuli FC, Kwasi alifanikiwa kufunga mabao 5 katika mechi 11 za ligi kuu Tanzania bara alizocheza kabla ya dirisha dogo.

Hata hivyo, kwasasa Asante Kwasi ana jumla ya mabao 6 nyuma ya Emmanuel Okwi mwenye mabao 8 katika VPL na Habibu Kiombo mwenye mabao 7 kwenye VPL.

Trump akivuruga kitabu kinachomkosoa
Kalemani aifunda Tanesco