Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Zaituni Msofe amesema Serikali kwa kushirikiana na vyama vya ushirika inaendelea na mpango wa kudhibiti biashara haramu ya uuzaji, ulanguzi na utoroshaji wa kahawa kwa njia za magendo ambazo ni kinyume na utaratibu.
Zaituni ameyasema hayo katikq mkutano Mkuu wa chama cha ushirika cha KDCU kinachojishughulisha na ukusanyaji wa Kahawa Wilaya za Karagwe na Kyerwa kwa kupitia vyama vya ushirika vinavyowawezesha wakulima kupata fedha za kukimu mahitaji ili wasiuze kahawa kimagendo.
Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Zaituni Msofe
Amesema, “bado kuna kata hazijakusanya zote zilitorosha tukasema tutafute mbinu zingine ya kuweza kudhibiti hili swala, ndio tukaja na hili wazo la kusema sasa wenzetu wa KDCU wazisaidie zile AMCOS zilizopo mipakani kwa kuwapa fedha,”
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Inosent Bashungwa akizungumza na wakulima wa zao la Kahawa.
“Tukielewa kwamba wenzetu wanatorosha kwa kufata pesa lakini pia kuna kipindi kingine unamkuta mtu ana shida anataka fedha kutatua shida yake ya haraka kwahiyo huyo anaweza kupewa fedha kiasi kwa makubaliano yatakayokuwa yamepitishwa,” aliongeza Mkuu huyo wa Wilaya.
Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Inocent Bashungwa amesisitiza wakulima kujihusisha kwenye uzalishaji wa tija kwa kuwatumia maafisa ugani, kupata pembejeo na mbinu za kisasa za kilimo.
Baadhi ya wakulima wa zao la Kahawa kutoka Wilaya ya Karagwe na Kyerwa wakiwa kwenye mkutano Mkuu wa KDCU.
Amesema, Mwelekeo wa zao la kahawa na mifumo ndani ya serikali inaendelea kuboreshwa, lazima tujikite kwenye uzalishaji wa tija eneo hilo hilo kama ulikuwa unapata gunia moja upate gunia tano.”