Klabu ya Osasuna itakumbana na adhabu kutoka Ligi Kuu Hispania (La Liga) baada ya mashabiki wa klabu hiyo kumdhihaki Mshambuliaji mpya Mason Greenwood wakati wa mechi mwishoni mwa juma lililopita.

Greenwood alirejea uwanjani baada ya kukaa nje kwa miezi 20 akiiwezesha Getafe kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Osasuna.

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wa Osasuna hawakufurahishwa baada Mshambuliaji huyo wa kimataifa England kuingia akitokea benchi zikibaki dakika 13 mpira kumalizika.

Greenwood alionekana mara ya kwaza baada ya miaka miwili kwani mara ya mwisho kucheza ilikuwa dhidi ya West Ham United kabla ya kushtakiwa mwaka jana kwa kosa la kutishia kuua na kubaka.

Baadhi ya mashabiki wa Osasuna walimuimba Greenwood kwa maneno ya chuki, lakini La Liga iliikemea Osasuna, na kuahidi kuichukulia hatua.

Mashabiki wa timu hiyo walilaani Getafe kumsajili Greenwood kwa mkopo kutoka Manchester United licha ya kesi yake kufutwa baada ya ushahidi kutotosheleza, Mashabiki walisusa kuingia katika Uwanja wa Colseum Alfonso wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 15600.

Kocha Azam FC afunguka pengo la Sebo
Ramani ya kutinga Makundi kuchorwa Chamazi