Mashabiki na hata viongozi wa Barcelona walitamani kuistaafisha jezi yao namba 10 kwa heshima ya nahodha wao aliyeondoka, Lionel Messi.

Lakini sheria na kanuni za La Liga zimewazuia kufanya hivyo.

Sheria hizo zinasema kila timu ya La Liga inapaswa kusajili wachezaji wasiozidi 25 wenye namba kuanzia 1 hadi 25.

Lazima kuwe na makipa wasiozidi watatu na watavaa jezi namba 1, namba 13 na namba 25.

Endapo kuna mchezaji kutoka timu ya akiba (Timu B) anatakiwa kutumika, basi apewe jezi kuanzia 26 hadi 50.

Kwa hiyo endapo wangeistaafisha, wangetakiwa kusajili wachezaji 24 tu, jambo ambalo lingekuwa tatizo kwao kwani wangekuwa na kikosi chembamba.

Hii imewalazimu kuendelea kuitumia jezi hiyo na sasa wamempa kijana kutoka akademi ya La Masia, Ansu Fati.

Barcelona ni kama wana mkosi na sheria za La Liga. Kisa cha kuondoka Lionel Messi ni sheria hizo hizo la La Liga ambazo zinakataza timu kutumia zaidi ya asilimia 70 ya pato lake kulipa mishahara.

Wafuatao ni wachezaji waliovaa jezi namba 10 ya Barcelona ndani ya miaka 40 na ushei, iliyopita.

1978/1979 Juan Manuel Asensi
1982/1984 Diego Maradona
1989/1990 Robert
1991/1992 Pep Guardiola
1991/1992 Richard Witschge
1993/1994 Hristo Stoichkov
1993/1994 – 1994/1995 Romário
1995/1996 Lluís Carreras
1995/1996 Roger García
1996/1997 – 1998/1999 Giovanni
1999/2000 Jari Litmanen
2000/2001 – 2001/2002 Rivaldo
2002/2003 Juan Riquelme
2003/2004 – 2007/2008 Ronaldinho
2008/2009- 2020/2021 Lionel Messi
2021/2022 – Ansu Fati

Nugaz awaaga Young Africans
Geita Gold kutumia Uwanja wa CCM Kirumba