Shirikisho la soka nchini Hispania limetangaza muda wa kuanza kwa mchezo wa mzunguuko wa 26 kati ya Real Madrid dhidi ya FC Barcelona, ambao umepangwa kuchezwa Machi Mosi kwenye dimba la Santiago Bernabéu.

Taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka Hispania imeeleza kuwa, mchezo wa wapinzani hao wakubwa ambao unajulikana kwa jina la El Classico, utanza mishale ya saa tatu kamili usiku kwa saa za nchi hiyo (Saa tano usiku kwa saa za Afrika mashariki).

Muda huo utakua sawa na ule wa mchezo wa mzunguuko wa kwanza, ambapo FC Barcelona walikua wenyeji dhidi ya Real Madrid, na kuambulia matokeo ya bila kufungana kwenye uwanja wa Camp Nou.

Kwa sasa wawili hao wamepisha alama tatu kwenye msimamo wa ligi ya Hispania (La Liga), huku Real Madrid wakiwa kileleni kwa alama 49, na FC Barcelona wanafuatia kwa kufikisha alama 46.

Hata hivyo kuelekea mchezo wa mzunguuko wa pili wa ligi ya Hispania (La Liga) Real Madrid watakua na kibarua kigumu zaidi, kutokana na mpambano wao dhidi ya FC Barcelona kutarajia kutanguliwa na mtanange wa ligi ya mabingwa barani Ulaya ambao utawakutanisha dhidi ya Manchester City ya England.

Mchezo huo wa ligi ya mabingwa utachezwa siku tano kabla ya Real Madrid hawajakutana na FC Barcelona kwenye dimba la Santiago Bernabéu, Machi Mosi.

Simba, Yanga, Azam FC zaiingizia serikali bilioni 1.7
Bukina Faso: Bunge lapitisha wananchi kupewa silaha waingie vitani