Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kumtaja Amy Coney Barrett kuwa jaji wa mahakama ya juu zaidi nchini humo kumrithi Jaji Ruth Bader.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, Trump amefanya maamuzi kuhusu mrithi wa Ruth na kujitapa amefanya chaguo bora.

Trump alionyesha kusitasita kumuweka wazi mteule wake jana jioni wakati aliporejea kutoka kwenye mkutano wa kampeni na alipoulizwa iwapo wabunge wa Marekani waliarifiwa kwamba amemteua Barrett, Trump alitabasamu na kuwajibu, “ndicho wanachowaambia? “Mtajua kesho”.

Hatua hii inampa Trump fursa ya kujiongezea muda katika wakati anapojaribu kuwaimarisha wafuasi wake kabla ya mdahalo unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo na mgomBea wa urais kutoka chama cha Democrat, Joe Biden.

Ufichuzi huo wa Barrett unapelekea wasiwasi wademocrats katika wakati ambapo chama hicho kinapambania kuirejesha mikononi mwake ikulu ya White House pamoja na baraza la seneti.

Diamond na Mimi mars mambo ni moto
15 wauawa katika shambulio Nigeria