Skendo ya Rkelly bado ni changamoto kwa mwimbaji huyo nguli ambapo amejikuta akiwa mpweke kutokana na kila mtu kumkimbia hadi kufikia label yake kuwa mbali na muimbaji huyo
Taarifa kutoka mtandao wa TMZ zimeripoti kuwa Label ya RCA Records imeamua kusimamisha kuachia ngoma za mwimbaji huyo hadi skendo yake ya unyanyasaji wa kingono itapomalizika
Chanzo cha karibiu cha mikataba ya Rkelly pamoja na label ya RCA/Sony imesema label hiyo haitatayarisha wimbo wowote mpya kutoka kwa kellz, haitoweka pesa kwenye mradi wake wowote pia haitaachia wimbo wowote mpya hadi skendo yake pamoja na shauri lilipo mahakamani mjini Atlanta Georgia kumalizika.
Mwanamziki huyo bado anaidai RCA/Sony kwani hivi karibuni alikuwa anashinda studio kutengeneza muziki chini ya mkataba na anahitajika kuachiwa albamu mbili chini ya lebo hiyo.