Mchezaji wa mpira wa kikapu wa klabu ya Lakers inayoshiriki Ligi ya NBA ya Marekani, Lamar Odom ameanika ukweli wa namna alivyojikuta amekuwa teja wa ngono na anavyojutia maisha hayo.

Odom ambaye aliwahi kuwa mume wa mwanafamilia wa The Kardashian, Khloe Kardashian ameeleza kupitia kitabu chake cha ‘Darkness to Light’ kuwa aliwahi kufanya mapenzi na wanawake takribani 2,000 ikiwa ni pamoja na makahaba.

Akizungumza katika hali ya majuto, alieleza kuwa tabia hiyo ya ulaibu wa ngono ndio uliosababisha akavunja ndoa yake na Khloe baada ya mrembo huyo kumkamata akiwa amemsaliti na kahaba mmoja.

“Nilikuwa na ulaibu wa ngono kwa muda mrefu nikijaribu kukumbuka,” alisema Lamar.

“Kulikuwa na wanawake wengi wacheza uchi. Haikuwa kitu kikubwa kwangu, lakini mara zote nilikuwa nikiwalipa, sikuwahi kufikiria kuwapunguza,” aliongeza.

Nyota huyo alikumbushia maumivu aliyoyapata wakati alipofumaniwa na mkewe Khloe ambaye walifunga ndoa mwaka 2009, wakatengana mwaka 2013 kabla ya kutalakiana rasmi mwaka 2016.

“Nilishitushwa sana na tukio la kufumaniwa na mke wangu, iliniumiza sana, nilitaka kurudisha muda nyuma lakini sikuweza. Nilitaka kujificha lakini sikuweza. Lakini dhambi ile mbaya ilikuwa ngumu kuificha, nilikuwa na tatizo kubwa,” alisema.

Odom alieleza kuwa tabia ya uteja wa ngono aliipata kutokana na kuwa na tabia ya kuangalia filamu za ngono na kwa bahati mbaya hakupata mshauri mzuri wa kumsaidia kuachana na tabia hiyo hadi ilipomgharimu baadaye.

Lamar akiwa na Khloe Kardashian

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 39 na watoto watatu, ameiambia TMZ kuwa ameachana na tabia hiyo ambayo ilimsababisha pia kuangukia kwenye matumizi ya dawa za kulevya.

Amesema kupitia kitabu hicho, amepaza sauti ya kuwataka wanaume wengine kuepuka tabia hizo ili kuepuka kuharibu maisha yao.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 17, 2019
China: Ghorofa laanguka na kuua