Beki kutoka nchini Ivory Coast Lamine Kone amefichua siri la kutaka kuondoka katika klabu yake ya Sunderland.

Kone amehojiwa na Sky Sports News HQ na kueleza ukweli wa suala hilo kwa kusema tayari ameshawasilisha maombi ya kutaka kuondoka Stadium Of Light katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Beki huyo ambaye alizaliwa jijini Paris nchini Ufaransa miaka 27 iliyopita, amefanya hivyo baada ya klabu ya Everton, kuwasilisha ofa ya Pauni milion 18 kwa lengo la kumuhamishia Goodison Park.

Hata hivyo ofa hiyo iliwekwa kapuni na viongozi wa Sunderland kwa misingi ya kutaka Kone aendelee kubaki klabu hapo.

“Juma moja baada ya ofa hiyo kutumwa, nilifanya mchakato wa kuwasilisha maombi ya kutaka kuondoka, kwa sababu ninahitaji kucheza katika changamoto mpya,” Alisema Kone.

“Mbali na kuwasilisha maombi kwa njia ya maandishi, pia nimeshazungumza na viongozi wangu kwa njia ya simu, kuonana nao uso kwa uso lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea.

“Kwa masikitiko makubwa sana naomba nisema kuwa, mimi sipo katika mipango ya meneja mpya David Moyes, hivyo sina njia nyingine zaidi ya kulazimisha kuondoka.

Kone alisajiliwa na Sunderland mwezi januari mwaka 2016 akitokea nchini Ufaransa alipokua akiitumikia klabu ya Lorient, na alisaini mkataba wa miaka minne ambao utafikia kikomo mwaka 2020.

David Alaba Aipotezea Real Madrid
Kala Pina akosoa wimbo mpya wa Chid Benz, adai amewaangusha mashabiki