Uongozi wa Klabu ya TP Mazembe ya Lubumbashi-DR Congo umemtangaza Kocha kutoka nchini Senegal Mamadou Lamine Ndiaye kuwa Mkuu wa Benchi la Ufundi la Klabu hiyo.

Saa kadhaa zilizopita TP Mazembe imethibitisha kumrejesha Kocha huyo ambaye aliwahi kufanya kazi klabu klabuni hapo miaka 13 iliyopita, akiipa mafanikio klabu hiyo mwaka 2010 kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika na kucheza Fainali ya FIFA Club World Cup huko Abu Dhabi ambapo Walipoteza mbele ya Inter Milan.

Kocha huyo anarejea klabuni hapo na kuanza upya, huku kikosi cha TP Mazembe kikishindwa kufurukuta kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na Kombe la Shirikisho Barani humo chini ya Kocha mzawa Mihayo.

Ujumbe wa klabu ya TP Mazembe ulioandikwa katika ukurasa wa klabu hiyo wa Mtandao wa Twitter

Kazi kubwa kwa Kocha huyo ni kuhakikisha anarejesha makali ya klabu hiyo ndani na nje ya DR Congo, huku akitarajiwa kufanya usajili wa baadhi ya wachezaji ambao wataweza kumsaidia katika kibarua hicho.

Mwishoni mwa mwaka 2022, Kocha huyo mwenye umri wa miaka 66, alihusishwa kujiunga na Simba SC, siku chache baada ya kuondoka Horoya AC ya Guinea, lakini baadae Klabu hiyo ya Dar es salaam-Tanzania ilimtangaza Kocha Robertinho.

Ndiaye amewahi kuzinoa klabu za Mulhouse (1998), Coton Sport (2003–2006), Maghreb Fez (2008–2009), TP Mazembe (2010–2013), Al-Hilal (2018–2019) na Horoya AC (2019–2022)

Mwaka 2008 alipata nafasi ya kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya taifa ya nchi ya Senegal.

Kobra azua kizaazaa ndani ya ndege, Rubani atua kwa dharula
Vipaumbele sekta ya Kilimo kuinua pato la Taifa, Mkulima