Baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu tangu kuanza kwa msimu huu, mabosi wa FC Barcelona wamemuongezea mkataba wa muda mrefu kinda wao matata, Lamine Yamal kwa ajili ya kusalia klabuni hapo.

Mabosi hao wamepanga kumpa mkataba mwingine Yamal ambao utamfanya abakie kikosini hapo hadi Juni 2026 ambapo mkataba huo utawekwa wazi Julai mwaka huu ikiwa ni baada ya kinda huyo kufikisha miaka 16.

Kando na Yamal pia FC Barcelona wamempa nyota wao mwingine, Alejandro Balde mkataba wa míaka mitano ambao wenyewe utamuweka kwa miamba hiyo hadi mwaka 2028.

Nyota hao wawili wamekuwa na msaada kwenye kikosi cha kocha Xavi Hernandez ndiyo maana wamepewa mikataba hiyo ambayo waliisaini kabla ya matayarisho kwa ajili ya msimu.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 19, 2023
EWURA yavifungia vituo vilivyoficha mafuta