Meneja wa Chelsea Frank Lampard amesema anahitaji ubora zaidi kwenye kikosi chake ili kufikia lengo la kufuzu kucheza michuano ya kimataifa Barani Ulaya msimu ujao.

Lampard ameyasema hayo baada ya kukishuhudia kikosi chake kikifanya vizuri usiku wa usiku wa kuamkia leo kwenye mchezo wa ligi Kuu ya England (EPL), kwa kuitandika Norwich City bao moja kwa sifuri.

Mshambuliaji Olivier Giroud ndiye aliyeipa matokeo chanya Chelsea kwa kufunga bao la kichwa akimalizia krosi ya nahodha wa Marekani Christian Pulisic, mpira uliomshinda mlinda mlango wa Norwich Tim Krul.

Licha ya matokeo hayo kuifanya Chelsea kujiimarisha kwenye nafasi ya tatu ya msimamo wa EPL inaonekana kutomridhisha Frank Lampard.

“Katika hatua hii kupata matokeo chanya ni muhimu mno, kutoruhusu goli ni jambo kubwa kwetu. Tunahitaji kuondoa mpira golini kwetu haraka, kushambulia haraka lakini bila kufanya hivyo inaweza kuwa hatari kwetu, ingawa bado matokeo chanya kipindi kama hiki ni muhimu zaidi, ili kupata nafasi ya ligi ya mabingwa Ulaya..

“Kuna muda ungwe ya pili, kama dakika 10 au 15 tulikuwa tunakaa na mpira bila sababu yoyote sikupendezwa tabia ile.” Alisema Lampard.

Norwich, ambao walishuka daraja rasmi Jumamosi iliyopita baada ya kukubali kipigo cha mabao manne kwa sifuri dhidi ya West Ham Utd hawakuwa kwenye ubora wowote Jan Jumanne licha ya Meneja kuwasifia kwa namna wanavyoendelea kujituma.

Ushindi wa Chelsea unatengeneza tofauti ya alama nne dhidi ya Leicester City na Manchester United zinazoshika nafasi ya nne na tano huku michezo miwiwli ikisalia kuhitimisha msimu wa EPL.

JPM atengua uteuzi wa Makonda na wenzake, Kunenge RC mpya Dar
Simba SC, Azam FC kumrudisha Kipre Tchetche